Loading...

Waziri Mbarawa asema wazee hawatakiwi TTCL

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema wakati umefika kwa wazee wanaofanya kazi katika Kampuni ya Simu ya TTCL, kuwaachia vijana kwa kuwa sekta ya mawasiliano hivi sasa ina ushindani mkubwa.

Akizindua nembo mpya ya kampuni hiyo na mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE jana, Profesa Mbarawa alisema wazee wamekuwa watu wa kuzungumza zaidi ofisini, kuliko kufanya kazi na kubuni mbinu mpya zenye kuhimili ushindani.

Mbarawa alisema uzinduzi wa nembo mpya katika kampuni hiyo, hautakuwa na maana ikiwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hawatabadilika na kutoa huduma zitakazowavutia wateja.

Aliishauri menejimenti kutoajiri watumishi kwa kujuana, bali watoe fursa kwa vijana wenye uwezo wa kuhimili ushindani unaotokana na mabadiliko ya teknolojia ya mawasiliano.

Akizungumzia maombi ya wananchi ya kutaka kusogezwa mbele kwa siku ya kuzima simu feki, waziri alisema Serikali haitasogeza mbele siku hiyo.

“Siku ya Juni 16, mwezi ujao Serikali itazima simu na vifaa vingine vyaIn mawasiliano feki bila kuongeza muda, huu ni muda wa watu kujiandaa,” alisema.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo, Edwina Lupembe alisema TTCL wakati wowote kuanzia sasa itaanzisha huduma ya usafirishaji wa fedha kama zilivyo kampuni nyingine za mkononi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema mabadiliko ya nembo hiyo yametokana na kampuni hiyo kuongeza huduma zinazotolewa kwa wateja.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top