Mimi ni mmoja wa wahanga wa Vyuo hivyo vikuu VISHIRIKI vilivyosajiliwa kutoka kwenye vyuo Vikuu na kujitegemea kuwa Vyuo vikuu huku wahitimu wakiwa hawajui walisoma vyuo gani.
Mfano mzuri kabisa mimi nimesoma Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini cha Sebastian Kolowa(SEKUCo) cha Lushoto, Tanga mwaka 2012 nikahitimu, lakini leo chuo hicho kimejitoa Tumaini na kuwa Chuo Kikuu cha kujitegemea yaani Sebastian Kolowa Memorial University(SEKOMU). Cha kushangaza leo mimi chuo nilichosoma kimefutwa yaani hakipo, tumebaki Tumaini jina ambako hakuna SEKUCO tena wala hiyo Shahada haipo tena bali imehamia SEKOMU ambako mimi sikusoma. Leo hii hata nikitambulisha kuwa nilisoma SEKUCO naonekana muongo maana chuokilichopo kwasasa siyo SEKUCO ni SEKOMU. Je, kwanini kama chuo kimebadili jina na mfumo na kujiondoa Tumaini na kufuta jina la chuo cha awali(College University),kwanini sasa tusibadilishiwe Vyeti Vyetu vya Shahada kutoka Sebastian Kolowa University College of Tumaini University kwenda Sebastian Kolowa Memorial University.
Nakumbuka wakati Chuo Kikuu Cha Mzumbe kinaanza kutoka Mzumbe IDM wale wote waliosoma Mzumbe IDM walitangaziwa kupeleka vyeti vyao Chuoni hapo na kubadilishiwa jina la chuo na pia wakabadilishiwa kutoka Advanced Diploma kwenda Bachelor Degree kulingana na mabadiliko ya chuo ya wakati huo. Ikiwa Mzumbe University waliliona hilo bado mapema na wakafanya mabadiliko ili kulinda wahitimu wao maana leo mtu ukimuuliza chuo cha Mzumbe IDM hajui bali anajua Mzumbe University.
Sasa hivi kuna Vyuo vingi tu, vishiriki ambavyo vimejitoa kwenye vyuo Vikuu vilivyokuwa na kuwa Vyuo Vikuu vya kujitegema huku kukiwa hakuna miundombinu ya kuwarekebishia Vyeti watangulizi wa vyuo hivyo,huku vyuo vikianzishwa bila kuangalia nani ana athirika, hii ni dhahiri kuwa Vyuo utitiri viko kwa ajili ya Biashara na sio kusaidia Taifa Letu Tanzania. Leo watoto wangu wakiwa watu wazima hawatajua chuo nilichosoma maana kimefutwa.
Na kumbuka pia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilikuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), lakini kilipojitegemea na kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam naamini wahitimu wake walibadilishiwa Vyeti kutoka Ushiriki wa Makerere kwenda Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Mimi ni Mtaaluma tena Mwalimu nasio Mwanasiasa maana wanasiasa ni Waongoooo, hawana data bali wana kick za kutokea kifursa. Ndugu Waziri wa Elimu nakuomba wakati unachamba na kuwauumbua watendaji wa TCU angalia pia na sisi tunavyoathirika na mfumo huu maana sasa hatuna vyuo, hata vyeti vyetu sasa si vyeti tena. Kama binadamu natanguliza samahani kwa wale niliowakwaza kwa makala hii, ila tujaribu kutafakari kwa kina maana mpaka sasa tangu tumalize chuo mwaka 2012 hatujajulishwa kwa lolote lile. Tunaomba kurudishiwa vyuo Vyetu kama hawawezi kutubadilishia muundo wa vyeti kuendana na mfumo mpya.
Ndimi Mjinga Namba Moja Tanzani
DEOGRATIUS KISANDU
Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu.
26/5/2016.
Post a Comment