Loading...

RAIS MAGUFULI AUWASHA MOTO TAKUKURU AWATIMUWA KAZI HAWA WAFANYAKAZI WALIOSAFIRI NJE YA NCHI BILA KIBALI

 Magufuli
Katika hatua nyingine katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
16 Desemba, 2015

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top