Loading...

Watanzania wawili watajwa jarida la Forbes






Watanzania wawili, Edwin Bruno na Nuya Hellen Dausen wametajwa katika jarida la Forbes Afrika kama wajasiriamali wenye umri wa chini ya miaka 30, wanaopewa kipaumbele kuwa mabilionea siku za usoni.


Kila mwaka jarida hilo hutoa orodha ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 30, wajasiriamali ambao wana nafasi ya kuwa mabilionea hapo baadaye.


Bruno ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Smart-code inayotoa huduma ya usomaji wa magazeti kwa njia ya mtandao, ametajwa katika jarida la Forbes Afrika mwaka huu.


Nuya, aliyewahi kuwa Miss Universe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Nuya Essence, kampuni inayotengeneza bidhaa za ngozi na vipodozi.


Majina ya wajasiriamali hao yalikusanywa na kuandaliwa na mhariri wa Forbes Afrika Ancillar Mangena ambaye naye ana umri chini ya miaka 30.


Akizungumzia kutajwa kwake katika jarida hilo, Bruno alisema: “Nimepewa heshima kubwa kuwa kwenye orodha hiyo, hata hivyo hii inatokana na juhudi za timu nzima pale Smart Codes.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top