Loading...

Mnyika: Sera ya madini ina kasoro

 Mbunge wa Kibamba, John Mnyika
KAMBI rasmi ya upinzani imeitaka serikali kurekebisha sera katika Sekta ya Madini, kwa kuwapa kipaumbele wazawa kuliko kuwapendelea wageni, anaandika Happiness Lidwino.
Akisoma hotuba leo bungeni John Mnyika, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Nishati na Madini juu ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 amesema, kama nchi inaweza kutumia rasilimali zake kama dhamana,  haina haja ya kuingia ubia na wageni.
“Kama tunaweza kutumia rasilimali zetu kama dhamana ni kwanini tuingie ubia na tusitoe ajira kwa wataalamu waliobobea katika fani hizo na sisi tukawa na umiliki wa asilimia 100?” amehoji Mnyika.
Katika hotuba hiyo ya Kambi Rasmi ya Upinzani inasema mikataba ya jinsi hiyo ndiyo itakayoliangamiza taifa kwa kuwa wataalam wanaoingia mikataba ya namna hiyo wanatakiwa kuwa maofisini.
Katika hotuba hiyo Mnyika amesema, Nchi hii  imejaaliwa wingi wa madini ya kila aina, hata hivyo, madini hayo hayatawasaidia wananchi kama hatua madhubuti hazitachukuliwa dhidi ya mapungufu yaliyomo kwenye sera ya madini inayojenga mazingira mazuri kwa wageni kumiliki utafutaji na uchimbaji madini hapa nchini dhidi ya ushiriki wa wazawa.
Ametaja baadhi ya mapungufu ambayo serikali inatakiwa kurekebisha kuwa ni, Serikali haikutakiwa kukabidhi utafutaji na uchimbaji madini mikononi mwa sekta binafsi ndani ya utandaawazi ulimwenguni, pasipo kuzingatia kuwa sekta binafsi ya Tanzania bado ni changa kushindana na makampuni ya kimataifa.
Pia haikutakiwa kuwalipisha wazawa na wageni ada na tozo sawa kwenye madini kama vile wageni wana haki sawa na wazawa, kwenye rasilimali zinazopatikana nchini Tanzania.
Amesema,  Serikali haikutakiwa kutumia misamaha ya kodi kwenye sekta hiyo  kama njia ya kuvutia wawekezaji badala ya kutengeneza mazingira wezeshi, kama vile nishati na miundombinu ya uhakika katika maeneo ya uchimbaji na hivyo kupelekea sekta kutokutoa pato stahiki kwa nchi.
“Serikali inapaswa kutambua kuwa, japokuwa wizara hii ina majukumu makubwa ya kuhakikisha rasilimali ya madini iliyopo hapa nchini, ile ambayo imeanza kuvunwa na ambayo hadi sasa haijaanza kuvunwa inatumika katika hali ambayo inatakiwa iwanufaishe watanzania wa sasa na wale ambao hawajazaliwa ili watanzania wajivunia mali zao kuliko kuzimalizia kwa wageni” amesema Mnyika.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top