Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
anafanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ili
kuondoa wasiwasi wakati ambapo taifa hlo linajiandaa kwa uchaguzi mwaka
mkuu ujao.
Bw Odinga alikatiza ziara yake ya kushiriki katika
mazishi kusini magharibi mwa eneo la Natol ili kuhudhuria mkutano huo wa
Uhuru Kenyatta katika mji mkuu wa Nairobi.''Nilipokea simu kutoka ikulu ya mkutano na rais Uhuru Kenyatta.Naomba ruhusa yenu watu wa Narok nielekee kuzungumza naye,alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akiwaambia waombolezaji.Nitatangaza kwa Wakenya iwapo tumekubaliana na iwapo hatujakubaliana pia nitawaelezea'', aliongezea bw Odinga.
Muungano wa upinzani nchini Kenya Cord umeapa kuhudhuria mkutano jijni Nairobi hapo kesho,licha ya kwamba serikali ilitangaza kupigwa marufuku.
Watu kadhaa wameuawa katika ghasia kati ya polisi na wafuasi wa upinzani wanaopigania mabadiliko ya sheria ya kupiga kura.
Post a Comment