Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Rais Mstaafu wa
Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutumia ibara ya 45 ya Katiba kutoa
msamaha kwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya
Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), wanaoelezwa kuamriwa
kurejesha fedha walizochukua.Aidha, alisema pale ambapo kuna makosa,
Rais anaweza kumsamehe mtu ambaye tayari amehukumiwa au kupewa adhabu
kwa kutumia ibara hiyo.Alisema, “Mimi kwa taarifa nilizonazo Mheshimiwa
Rais mstaafu hakutumia kifungu hicho,” Dk Mwakyembe alisema bila kueleza
kifungu kilichotumiwa.Alisema hivyo jana bungeni mjini hapa, wakati
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF)
aliyetaka kujua endapo Rais aliyepita alitumia madaraka yake vibaya,
alikosea au alikuwa sahihi kuruhusu baadhi ya watuhumiwa walipe fedha
walizodaiwa kuzifanyia ubadhirifu kupitia akaunti ya EPA
(Hawakutajwa).Pia, mbunge huyo katika swali lake la pili la nyongeza
alitaka kujua ni lini watafikishwa mahakamani akieleza kuwa msamaha
waliopewa haukuwa wa kikatiba na kwamba wanastahili kushitakiwa.Katika
swali lake la msingi, Haji alitaka kujua iwapo Rais ana mamlaka ya
kisheria kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambayo
mashauri yake yapo katika vyombo vya dola kwenye hatua za uchunguzi,
upelelezi au mahakamani.
Loading...
Post a Comment