Loading...

Muhtasari: Habari kuu leo Ijumaa

Miongoni mwa habari nyingine kuu leo, msichana mwingine wa Chibok ameokolewa, mkuu wa polisi San Francisco akajiuzulu na Clinton anasema hawezi kushindwa na Sanders.

1. Wanawake 100 waokolewa kutoka kwa Boko Haram

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaokoa karibu wanawake na wasichana 100 waliokuwa wakizuiliwa na wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Borno, kufuatia operesheni kali iliyofanywa katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria.
Miongoni mwao ni mmoja wa wasichana mia mbili waliotekwa kutoka shule ya Chibok mwaka wa 2014. Msichana huyo ni wa pili kuokolewa tangu wasichana hao walipotekwa nyara.

2. Mabaki ya ndege ya EgyptAir yaendelea kusakwa

Image copyrightGETTY
Huku shughuli ya kutafuta mabaki ya ndege ya shirika la EgyptAir, iliyotoweka na kuanguka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterenian, Utawala nchini Ufaransa unajaribu kubainisha ikiwa kulikuwepo na utepetevu wa kiusalama katika uwanja mkuu wa ndege mjini Paris.
Ndege hiyo aina ya Airbus ilitoweka ikiwa safarini kuelea Cairo kutoka Paris, ikiwa na watu 66.
Waziri anayehusika na safari zake ndege nchini Misri amesema kuna uwezekano mkubwa ajali hiyo ilisababishwa na kitendo cha kigaidi kuliko hitilafu za kimitambo.

3. Rais mwanamke aapishwa Taiwan

Image copyrightAP
Rais wa kwanza wa kike wa Taiwan, ameapishwa hivi leo katika sherehe zitakazofanyika katika mji mkuu wa Taipei.
Tsai In-wen, ambaye chama chake kinataka uhuru kutoka Uchina, alishinda na idadi kubwa ya kura katika uchaguzi uliofanyika Februari mwaka huu.
Ushindi wake umeathiri uhusiano wa taifa hilo na utawala wa Beijing.

4. Mkuu wa polisi San Francisco ajiuzulu

Image copyrightGETTY
Afisa mkuu wa polisi mjini San Francisco, Greg Suhr, amejiuzulu saa chache baada ya afisa mmoja wa polisi kumpiga risasi na kumuua mwanamke mmoja mweusi ambaye alikuwa akiendesha gari lililokuwa limeibiwa.
Afisa huyo na idara yake zimeshutumiwa kwa kuhusika na vifo vya washukiwa kadhaa wenye asili ya Kiafrika.

5 Clinton asema hawezi kushindwa na Sanders

Mgombea anayeongoza wa chama cha Democratic katika uteuzi wa Urais, Bi Hillary Clinton amesema, hakuna kitakachomzuia kuteuliwa kuwa mgombea wa chama hicho, katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu.
Clinton anasema kufikia sana anaongoza na idadi kubwa ya wajumbe kuliko mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders.

6. Mahakama yaunga mkono uamuzi wa Maduro

Image copyrightGETTY
Na mahakakama ya juu zaidi nchini Venezuela, imeamua kuwa agizo lililotolewa na rais wa nchi hiyo la kutangaza hali ya hatari nchini humo lilikukiuka katiba ya nchi.
Hatua hiyo ya mahakama inampa nguvu zaidi za kujiongezea mamlaka zaidi anapoendelea kukabiliana na mzozo wa kiuchumi unaokumba taifa hilo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top