Loading...

BREAKING NEWS: TAARIFA ZAKUSIKITISHA, SERIKALI YATOA TAMKO HILI KALI SANA HUKO BUNGENI, HAKUNA MTU KUSIMAMA NDANI YA GARI >>>HII HAPA TAARIFA RASMI

SERIKALI imesema ni kosa kwa mtu yeyote kutokuwa na kiti cha kukaa ndani ya basi na hivyo atakapokutwa amesimama atahesabiwa kuwa alikuwa amening’inia ndani ya gari.
Hayo yalielezwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Fakharia Shomari Khamisi (CCM).
Mbunge huyo alitaka kufahamu iwapo serikali haioni kuwa kutoza faini na kuacha gari liendelee na safari wakati limejaza watu ni sawa na kuhalalisha kosa hilo.
“Serikali haioni kuwa ikiwashusha abiria waliozidi itakuwa imetoa fundisho na kupunguza ajali kwa abiria ambao hupanda huku wakijua limejaa?” Alihoji mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Masauni alisema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 Kifungu cha 58, ni kosa kwa abiria au mtu yeyote kutokuwa na kiti cha kukaa ndani ya gari la abiria na hivyo mtu huyo atahesabika kwamba amening’inia ndani ya gari hilo.
“Mabasi yanayotozwa faini kwa kuzidisha abiria yakiwa vituoni na maeneo salama, abiria waliozidi hushushwa na kurudishiwa nauli zao na utaratibu wa kuwatafutia mabasi mengine yenye nafasi hufanywa,” alisema Massauni.
Aidha, alisema kama mabasi hayo yatakamatwa katika maeneo ambayo si salama, huachwa yakaendelea na safari kisha mawasiliano hufanyika katika vituo vya polisi vilivyopo mbele ili abiria washushwe kwenye maeneo ambayo ni salama kwao.
Katika swali la nyongeza la Mbunge huyo aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuanzisha mfuko wa majanga ya ajali na kuwatoza faini abiria waliosimama, Massauni alijibu kuwa mambo hayo ni mazuri kwa kusaidia kupunguza ajali hizo na kwamba serikali itayafanyia kazi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top