Bodi ya Sukari Tanzania imetangaza bei elekezi ya sukari kuwa ni Sh. 1,800 kwa kilo moja na yeyotye ambaye atakiuka agizo hilo atachukuliwa hatua.
Awali sukari ilipanda bei na kufikia Sh. 2,500 kwa kilo mara tu baada ya
agizo alilolitoa Rais Dk. John Magufuli la kusitisha vibali vya
uagizaji sukari kutoka nje ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini, Henry Semwaza, alitangaza
uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam na
kuelea kuwa bei hiyo inatakiwa kuanza kutumika mara moja kwenye maduka
yote nchini.
Alisema kwa sasa hakuna uhaba wa sukari kwenye maghala ya kuhifadhia bidhaa hiyo kama inavyoenezwa.
Semwaza alisema wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hilo
pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa
wananchi bila kuhodhi.
Alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali kwa wauzaji ambao watakaidi agizo hilo la bei elekezi.
“Wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hilo pamoja na
kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi
bila kuhodhi,” alisema
Aidha, alisema maafisa wa bodi hiyo kwa kushirikiana na mamlaka zingine
za serikali kote nchini hususan maafisa wa biashara wa mkoa na wilaya
kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment