WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakihaha kuendesha propaganda chafu kuhalalisha uchaguzi haramu, Chama cha Wananchi (CUF) kimefanikiwa kuteka wanachama wake, anaandika Michael Sarungi.
“Wanahaha na hawatafanikiwa, tumeweza kushikamana na kusimamia kamba moja ya kupuuza uchaguzi wa CCM na ZEC, tumeruka mitego mingi na sasa hawaamini,” anasema Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Bara na kuongeza;
“Wamefanya mengi lakini tunashukuru kihunzi hiki tumekiruka na sasa wanataka kuwavuruga wawakilishi na wabunge wa CUF, wamechelewa sasa.”
Jana kumeendeshwa propaganda kuwa, wabunge na wawakilishi wa CUF Tanzania bara na Visiwani wamejivua Ubunge na Uwakilishi kwa madai ya kupinga uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kesho.
Kwa mujibu wa barua feki iliyosambazwa kwenye mitandao iliarifu kuwa wabunge na wawakilishi hao wamehiyari kuachia nafasi zao wakilenga kuupinga uchaguzi huo.
Barua hiyo inaonekana iliandikwa Machi 17 kwenda kwenye ofisi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ikonekana kuwa ilisainiwa na Ahmed Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu CUF kisiwani Zanzibar.
Sakaya amesema, ni propanganda za CCM kwani chama chao hufanya uamuzi mzito kupitia vikao vya Baraza Kuu ambavyo havijaitishwa.
Amesema (CUF) ni chama kinachofuata misingi na taratibu za kikatiba ndani ya chama na kuwa, aumuzi mgumu kama huo hauwezi kutolewa na mtu binafsi bila ya vikao vya chama.
“Hizi ni taarifa ambazo hazina ukweli wa aina yoyote mpaka leo wabunge wetu walikuwa wanaendelea na vikao vya kamati hata sisi hatujui hizi habari zimetoka wapi,” amesema Sakaya.
Amesema watu wanaoeneza upuuzi kama huo wanapaswa kulaaniwa na wapenda demokrasia wote ndani na nje ya chama kwa maslahi mapana ya chama na nchi kwa ujumla.
Post a Comment