Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.
Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama kuna faida au hasara kwa wananchi.
“Natoa tamko kwamba huduma hii iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani wananchi” alisisitiza Bi. Mwalimu.
Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hapo kwa kulipia shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu kumi ya kumuona daktari , elfu kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni kwa malipo ya chakula kwa wiki.
“Huduma hii inalenga kuwasaidia wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa na kupunguza usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta vyakula hospitalini ili kuimalisha afya zao kwa ujumla”aliongeza Bi.Mwalimu.
Post a Comment