Mlipuko mkubwa
umekumba hoteli moja katikati ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuna
sauti za ufyatulianaji wa risasi katika kile kinachoaminika huenda ni
shambulio la wapiganaji wa al-Shabab.
Kulingana na mwandishi wa
BBC Ibrahim Aden mjini Mogadishu, mlipuko huo ulikumba hoteli ya Naso
Hablod ikiwa ni hatua chache kutoka kwa uwanja wa ndegewa mji huo.Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Ripoti zinasema kuwa huenda kulikuwa na mlipuko wa pili.

''Walianza na mlipuaji wa kujitolea muhanga na baadaye kuvamia.Kwa sasa wako ndani na ufyatuliaji mkubwa wa risasi unaendelea'' ,alisema msemaji wa polisi meja Nur Farah.
Post a Comment