Uingereza imetoa msimamo wake kwamba
itapeleka meli na askari wa majini kutoka katika ufalme wake nchini
Libya ili kusaidia kutoa mafunzo kwa walinzi wa pwani wawe na uwezo wa
kuzuia biashara ya ulanguzi kwa watu wanaotaka kuvuka bahari ya
Mediterranean.
Maofisa hao wameeleza pia kuwa wanatafuta kibali
cha umoja wa mataifa kwa ajili ya meli ya kuzuia boti za magendo ya
silaha dhidi ya kundi Islamic State.Mapema, wahamiaji kadhaa wa kadhaa walihofiwa kuzama wakati mashua zao zilizo kuwa na msongamano mkubwa zilipopinduka pwani ya Libya.
Walinzi wa pwani ya Italia wanasema kwamba hatua hiyo imesaidia kuokoa maisha ya wahamiaji elfu nne waliokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean wiki hii
Post a Comment