Loading...

PICHA ZINATISHA:..RISASI ZALINDIMA DAR WATU WAWILI WAUAWA, MAJAMBAZI YA YAVAMIA BANK YA CRDB NA DCB BANK HUKO CHANIKA

Majambazi wamevamia na kupora pesa CRDB na DCB Bank huko Chanika. Wadaiwa kuua kwa risasi watu 2 na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi.
-Wahalifu hao walianza kuingia kwenye Benki ya DCB na kupora fedha zilizokuwa kaunta baada ya hapo walivamia Benki ya CRDB na kupora fedha hadi sasa haijajulikana ni kiasi gani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Ulrich Matei, ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa tukio hilo na kwamba majambazi hao wanasadikiwa kuwa walikuwa kati ya 6 hadi 8.
Amesema wahalifu hao walianza kuingia kwenye Benki ya DCB na kupora fedha zilizokuwa kaunta na muda mchache baada ya hapo walivamia Benki ya CRDB na kupora fedha ambazo hadi sasa haijajulikana thamani yake.
Aidha, amesema majambazi hao waliwaua askari wawili wa Suma JKT, waliotambuliwa kwa majina ya Ramadhani Halidi na Shane Rajabu.
"Tumeanza upelelezi ikiwemo kuelekea katika maeneo ya Mkuranga ambapo ndiko tunakoamini kwamba hawa wahalifu wameelekea, tutakapowakamata tutawapa taarifa kamili" alikaririwa na JamiiForums.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top