Loading...

Wanandoa Waliodumu Muda Mrefu Kuanza Kupewa Tuzo Tanzania


Imezoeleka kwamba ndoa za kikatoliki zikifungwa zimefungwa lakini pamoja na sharti hilo idadi ya ndoa zinazovunjika inaendelea kuongezeka ambapo sasa kanisa katoliki limekuja na hii ya kuanzisha tuzo maalumu kwa Wanandoa wakongwe zaidi kwa mwaka huu katika kanisa hilo.
BBC SWAHILI wameripoti kwamba Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es salaam limeandaa kliniki ya ndoa ili kuweza kuwapa fursa Wanandoa kuimarisha ndoa zao kiimani, Padre Novatus Mbaula ambaye ni mkurugenzi wa ndoa na familia anaeleza lengo la kliniki hii ni kuwapa nafasi wanandoa kupata neno la Mungu na kuweza kuongea juu changamoto zao mbalimbali kuongea kuhusu maisha yao ya ndoa.
Ni nafasi ambayo wanandoa ambao wana uzoefu mkubwa katika ndoa wanaweza kuwafaidisha wanandoa wachanga na miongoni mwa watu waliohudhuria kliniki hii ni wanandoa wenye ndoa yenye miaka 61, Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbena mwenye umri wa miaka 86 alifunga ndoa akiwa na miaka 25 mwaka 1965 June,anasema wao zamani walikua wanafuata mtu na familia gani na ina vigezo gani.
Walikua wanaangalia tabia kama msichana hana tabia nzuri huoi huko, kama familia ina watu walevi bali unatafuta familia yenye watoto wenye tabia nzuri ili na wewe uweze kupata watoto wenye tabia nzuri.
S

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top