Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imetangaza tarehe yake ya kufanya uchaguzi, huku ikisisitiza kutotambua mamlaka ya usimamizi wa uchaguzi wao kupitia Kamati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambayo nayo imepanga tarehe yake.
Kikao hicho kitakachokutanisha pande tatu, TFF, Yanga na Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) kitafanyika leo, Dar es Salaam.
Taarifa zilizopatikana jijini zilidai kuwa dhamira ya kikao hicho ni kutafuta suluhu ya kumaliza malumbano yanayoendelea kuhusu uchaguzi wa klabu hiyo ya Jangwani.
Katika kuonyesha uchaguzi huyo wa Yanga 'unaogopwa', mvutano huo ambao umekuwa gumzo kuanzia wiki iliyopita na kusababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Aloyce Komba kujitoa, suala hilo halikujadiliwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana jana jijini.
"Kesho (leo) kutakuwa na kikao cha pande tatu, Kamati ya Utendaji halikujadili chochote," alisema mjumbe mmoja wa kamati hiyo iliyoko chini ya Rais Jamal Malinzi.
Naye kiongozi mwingine alisema walishangaa suala la Yanga kutokuwa sehemu ya ajenda zilizojadiliwa kwenye kikao hicho, wakati shirikisho limetajwa kukosa 'nguvu' katika uchaguzi huo kama ilivyokuwa kwa wanachama wengine.
"Uchaguzi wa Yanga haukujadiliwa na wala haukuonekana ni ajenda, na sisi wengine tunaona hatuna sababu ya kuuliza," alisema mjumbe mwingine (jina linahifadhiwa).
USAILI WAFANYIKA
Wagombea 19 waliopitishwa walipitishwa chini ya sekretarieti ya klabu walishiriki katika usajili kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uchaguzi utakaofanyika Jumapili Juni 11.
Orodha ya majina ya wagombea hao itatolewa leo na miongoni mwao ni Clement Sanga anayewania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, huku wanaowania nafasi nane za Kamati ya Utendaji ni pamoja na Samuel Lukumay, Salum Mkemi, Beda Tindwa, Lameck Nyambaya, David Ruhago na Ayoub Nyenzi.
Wengine ni George Manyama, Silvester Haule, Siza Lyimo, Hussein David, Hashim Mdhihiri, Athumani Kihamia, Pascal Laizer, Godfrey Ayoub, Bakari Malima, Mchafu Ahmed na Thobias Lingalangala.
Juni Mosi TFF ilisisitiza kuwa kamati yake ndiyo itasimamia uchaguzi wa Yanga Juni 25 na siyo Juni 11 kama Yanga wanavyotaka.
Post a Comment