Rais wa Marekani,Barack Obama
amesema shambulio la risasi katika Klabu ya usiku mjini Orlando ni la
kigaidi na ni kitendo cha chuki
Takriban watu 50 wamepoteza maisha
na wengine 53 wamejeruhiwa siku ya Jumapili, baada ya mtu mmoja
aliyekuwa na silaha kufyatulia risasi Klabu moja ya usiku iliyokuwa
ikiwakutanisha watu wa mapenzi ya jinsia moja mjini Orlando nchini
Marekani.Polisi nchini humo wamesema kuwa ni shambulio baya kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Rais Obama amesema Marekani inaungana ikiwa na huzuni,mshtuko mkubwa na inalenga kutetea watu wake, pia amesema mauaji hayo yanawakumbusha ni namna gani ilivyo rahisi kupata silaha hatari nchini Marekani.
Shirika la kijasusi nchini humo,FBI limemtambua mshambuliaji huyo kuwa raia wa Marekani,Omar Mateen ambaye naye aliuawa wakati wa mapambano na vikosi vya usalama katika klabu hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya watu 300 ndani yake.
Post a Comment