Loading...

BREAKING NEWS: MSIBA WA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DARA "WILSON KABWE" WAIBUA MAZITO HIVI NDIVYO MKUU WA MKOA WA DAR PAUL MAKONDA ALIVYOCHUNIWA MSIBANI NA MTOTO WA KABWE



Siku ya jana ilikua ni siku ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndg. Wilson Kabwe iliyofanyika viwanja vya Karimjee katikati ya Jiji la Dar es salaam.
Katika hali ya kutoelewa nini kinachoendelea, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alijikuta akiganda kwa sekunde kadhaa mbele ya binti wa marehemu Wilson Kabwe anayefahamika kwanjina la Anna pale alipo jaribu kumpa mkono wa pole lakini binti huyo alikataa kujibu huku akibubujikwa na machozi ya uchungu.
Habari kutoka kwa watu karibu wa familia zinasema binti huyo alifanya hivyo kutokana na machungu aliyokuwa nayo juu ya Makonda ambae wiki za usoni inaeleweka ya kwamba Mkuu huyo wa mkoa alikuwa mstari wa mbele kuchochea moto ambao ulisababisha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo .
Habari za ndani zinasema kitendo hicho cha binti huyo cha kukataa mkono wa Makonda kimetokana na hotuba aliyotoa Mh. Makonda ambayo kwa maudhui ilikua imejaa utukufu binafsi ya kitendo alichofanya akisema "Kaka yangu kabwe ameondoka lakini huu sio mwisho wa kupambana na mafisadi".
Mpaka habari hizi zinatufikia tulijaribu kuwasiliana na msemaji wa familia lakini jitihada zetu ziligonga mwamba kwani alikua hapatikani.. Source: Tz Daima

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top