Taarifa
kuwa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam iliidhinisha na kutoa
fedha za ukarabati wa barabara hewa, haipaswi kuachwa pasipo kujadiliwa.
Jana,
gazeti hili lilichapisha taarifa ya kushangaza kuhusu Meya wa Manispaa
ya Kinondoni, Boniface Jacob kubaini matumizi ya Sh392 milioni
zilizoandikwa kwenye ripoti ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kukarabati
barabara ya Igesa - Sinza, jambo ambalo kwa mujibu wa meya halikufanyika.
Kilichofanyika kwa maelezo wa mchumi wa manispaa hiyo ni kuwa fedha zilizotolewa zilitumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma.
Post a Comment