Mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera amevitaka vyombo vya dola kuanza uchunguzi kwa kuwahoji Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang Bw Felix Paul Mabula na mafisa wengine watano mara baada ya kamati ya uchunguzi aliyounda kubaini kuwepo kwa tuhuma 13 za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yaliyosababisha ufujaji wa kiasi cha zaidi ya shilingi billioni moja na kukwamisha miradi ya maendeleo ya halmashauri hiyo.
Agizo hilo amelitoa wakati akiwasilisha taarifa hiyo kwa baraza maalum la halmashauri hiyo,wakuu wa idara,huku umati mkubwa wa wananchi ukifurika na baadaye kukabidhi taarifa hiyo yenye tuhuma 13 yenye mapendekezo 11 kwa Polisi na Takukuru ili kuanza kuwahoji akiwemo mhasibu wa Wizara ya afya Bw Fareed diwani akituhumiwa kugawana kiasi cha shilingi mil 44.6 za chanjo ya surua na rubela na kudai kamati yake imebaini kuwepo kwa madudu ya ufujaji huo kwa asilimia 100.
Hata hivyo Dr Bendera amewataja watuhumiwa watakaoungana na mkurugenzi huyo kuhojiwa kuwa ni mweka hazina Bw Mazengo Matonya,mhasibu wa matumizi Bi Welu Sambalu, Bw Mkojera Philemon Mkojera afisa idara ya afya na mtunza fedha Bw Marcel Siima,hatua ambayo mbunge wa viti maalum Bi Rose kamili amesema kamati hiyo kuelekeza nguvu zake kwa idara ya maji yenye upotevu wa shilingi mil 540 na kusababisha wananchi kukosa maji.
Kwa upande mwingine Dr Bendera mbali ya kuzitaka vyombo vya dola kuanza uchunguzi haraka,amesema kamati yake imetoa pendekezo la kuwajibishwa kwa watumishi wengine watatu akiwemo mwanasheria wa halmashauri sambamba na diwani wa CCM viti maalum Bi daines Peter anayedaiwa kuandaliwa ili kumshawishi mwenyekiti wa kamati hiyo kujenga mazingira ya kuacha kumvua madaraka mkurugenzi mtendaji huyo.
Post a Comment