Sisi wapinzani hatujawahi kuogopa mjadala halali bungeni hata siku moja.
Ushahidi ni kazi kubwa tuliyoifanya Bunge la Kumi na Bunge la Katiba.
Tatizo ni kwamba kwa sasa hakuna mjadala halali tena bungeni. Kwa
kutumia majority yao na kiti cha Spika, watawala wamehakikisha
hatuzungumzi bungeni. Ukitaka kuzungumza unakatazwa, ukibisha
unakabiliwa na mapolisi ndani ya Ukumbi wa Bunge au unafukuzwa kabisa.
The only choice we've is to put up and pay the price or to shut up and
be party to the illegitimate decisions. Kanuni kuu ya utendaji wa
mabunge ya dunia ni: 'give the minority a day and the majority a sway.'
Kwa Bunge la Tanzania kanuni hiyo kuu imetupwa pembeni, sasa ni
kuendesha Bunge kwa mabavu na ubabe mbele kwa mbele. Katika mazingira
haya, boycott is a very important weapon, it deprives the decisions of
any legitimacy. Tuungeni mkono. Wote, hata mlioko CCM, mnahitaji
upinzani wenye sauti bungeni. Hiyo ndio salama yetu wote. Sauti hiyo
ikizimwa tumekwisha wote.
Friday, June 24, 2016
Post a Comment