Waachane kupoteza muda kuvutana juu ya bunge kuwa laivu bali waangalie plan B .Kwa kuwa hata wafanyaje hiyo itakuwa hivyo kutokana na uchache wao ndani ya Bunge.
Plan B-wawafanyie kazi watu wao kwa kuisimamia Serikali vizuri katika maeneo yao ili yale matunda ndio iwe sera yao katika vyombo vya habari.
Mfano: Tumeona bajeti ya jimbo la kinondoni ni nzuri sana na kama itaenda kama ilivyopangwa basi utakuwa mfano nzuri na watu wataona umuhimu wa upinzani kuongoza jimbo.
Kama wataendelea kuvutana na serikali huku mambo yakiwa yanaenda pasipo kuona impacts za kugoma kwa wabunge wa upinzani basi serikali ambayo ipo chini ya CCM na huu moto wa mh rais serikali itazidi kujizolea sifa kwa kuwa wanacho kifanya wananchi wanakiona .
Ni upinzani kukaa na kujitathmini mapema sana bila ya hivyo watakuja kujitathmini wakati Mh rais yeye anasema jamani wananchi katika miaka yangu 5 nimefanya 1,2,3,4,5....naombeni tena mnipe miaka 5 nifanye 1,2,3,4,5...
Wakati huo wapinzani watabaki na mabomu (tuhuma za ufisadi mbalimbali) kwenye mikoba yasiyo na madhara ambayo wananchi wamechoka kuyasikia.
Siku hazigandi kama alivyoimba mwanamuziki mmoja maarufu nchini. Muda wa wao kufanya jambo la maana ndio huu.
Post a Comment