Loading...

Ni halali wapenzi wa jinsia moja kuchunguzwa kimatibabu Kenya

 
Mahakama moja nchini Kenya imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyokuwa ikipinga uhalali wa uchunguzi wa tupu ya nyuma kama idhibati ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja.
Mahakama kuu ya Mombasa imesema kuna sheria fulani nchini Kenya inayohalalisha uchunguzi kama huo kwa sababu za kutafuta ushahidi. Kwenye uamuzi wake, hakimu Mathew Emukule alisema kulikuwa na ruhusa fulani kwenye sheria za Kenya kuchunguza maumbile ya binadamu kwa lengo la kutafuta ushahidi wa hatia kama unajisi au kuficha madawa ya kulevya.
Aidha alitupilia mbali wazo kuwa uchunguzi kama huo unabagua kijinsia, akisema kuwa tupu ya nyuma si ya kijinsia bali ni ya utumbo. Aidha alisema uchuguzi kama huo ulikubalika kwani walalamishi walikubali kufanyiwa.
Hatua hiyo inajiri baada ya wanaume wawili kuwasilisha ombi la kikatiba wakisema walifanyishwa uchunguzi wa kimaumbile sawa na virusi vya ukimwi na hepatitis, walipokamatwa kwa shutma za mapenzi ya jinsia moja mnamo Februari mwaka jana.
Mapenzi ya jinsia moja ni hatia nchini Kenya, na adhabu yake ni kifungo gerezani kwa muda usiozidi miaka kumi na nne.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top