Loading...

BREAKING NEWS: CHADEMA WALIPUA TENA BOMU LA LUGUMI "RAIS MAGUFULI ANAYO SIRI YA KAMPUNI YA LUGUMI" NA HIVI NDIVYO WALIVYOFUNGUKA CHADEMA JUU YA SWALA HILI

 Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kuamini kwamba, Rais John Magufuli anayo siri ya Kampuni ya Lugumu na INFOSYS hivyo anapatwa kigugumizi kuchukua hatua,anaandika Happiness Lidwino.
Pia chama hicho kimeeleza kwamba, ni vema Rais Magufuli ajitokeza hadharani na kuwaeleza wananchi uhusiano wake na Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye kampuni yake ndiyo iliyofunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole katika Jeshi la Polisi nchini.
“Chama kina mashaka juu ya mahusiano yao kwani licha ya Kitwanga kutajwa mara kadhaa kuwa anahusika na mkataba tata wa Bilioni 37 kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises.
“Lakini bado ameziba masikio. Hivyo, akiendelea kuwa kimya serikali yake itaangushwa kupitia waziri mkuu wake,” Salim Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mwalimu amesema, inawezekana Rais Magufuli anamasirahi binafsi na kampuni hiyo na hivyo kushikwa na kigugumizi jinsi ya kutoa maamuzi.
“Ni kitu cha kushangaza sana kwamba hadi sasa bado hajatoa kauli yoyote. Yeye ni mtaalamu wa kutumbua majipu kwa kupata habari mitandaoni na kwa kusikia tu kama alivyofanya kwa Mkurugenzi wa Jiji lakini majipu yaliyokaribu yake anayaogopa,” amesema na kuongeza;
“Tunamashaka na utumbuaji majipu wake inawezekana anafanya hivyo kwa kulipiza kisasi na kuharibu urafiki wa marais waliopita, ama anajifanya kutumbua watu ili awaweke watu wake waliokuwa wakimsapoti kwenye kampeni.
“Kama kweli anafanya hakim bona majibu yanayomuhusu hayatumbui?” amehoji Mwalimu.
Mwalimu pia amemtaka Waziri Kitwanga ambaye anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni yaINFOSYS iliyotumika kufunga mashine za kuchukua alama za vidole (AFIS) , ajitokeze kujibu tuhuma hizo ama ama ajiuzulu kwa kuwa hana sifa za kuwa Waziri tena.
“Kama bado wanafichiana siri yeye na rafiki yake basi aige mfano kwa Edward Lowasa aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye alijiuzulu kwa kumstahi rafiki yake aliyekuwa akinuka usifisadi Rais Jakaya Kikwete. Kitwanga ajipime na ajitafakari na kujitoa kwenye uwaziri,” amesema Mwalimu.
Awali, zabuni ya mkataba huo ilitangazwa tarehe 22 Septemba 2011 na kusainiwa terehe 23 Septemba mwaka huo huo ndani ya siku moja mkataba ukasainiwa jambo ambalo ni hatari.
Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd ilipewa tenda na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh 37 bilioni.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 tu vya polisi ambapo tayari kampuni hiyo imelipwa Sh. 34 bilioni ikiwa ni asilimia 99 ya fedha za mkataba huo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top